Tuesday, 5 May 2015


Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani John Kerry  amesema Somalia  iliyoharibiwa  kwa  vita inaelekea  kuwa na hali bora ya baadaye  wakati  alipofanya  ziara  yake muhimu ambayo  ni  ya kwanza  kwa  mwanadiplomasia  wa  ngazi  ya  juu wa Marekani tangu tukio la kuangushwa  ndege ya  Marekani  chapa Black Hawk mwaka 1993 ambapo  wanajeshi 18 wa Marekani waliuwawa.
John Kerry  amekutana  na  rais wa  Somalia Hassan Sheikh Mohamud  leo pamoja  na  waziri  mkuu  na  viongozi  wa  majimbo katika  uwanja  wa  ndege  wa  Mogadishu.
Katika  ajenda  za  mkutano  huo mapambano  dhidi  ya  kundi  la  al-Shabaab  lilikuwa  suala  kuu, pamoja  na  majeshi  ya  Afrika na ndege za  Marekani  zisizokuwa  na  rubani.
Majeshi  hayo  na  ndege  hizo zimedhoofisha  uongozi  wa  kundi  la al-Shabaab katika  miaka  ya  hivi  karibuni  na  kuliacha  kundi  hilo bila  ya  maeneo  makubwa  ambayo  lilikuwa  linadhibiti, ama  fedha zinazohitajika  kujijenga  upya.

No comments:

Post a Comment